NINI MAANA NA TOFAUTI YA HAYA MANENO?

1. Kuungama

2. Kutubu

3. Kuomba Rehema

4. Kuomba Utakaso


Ohoooo… haya ni mambo ambayo wengi wetu tunakoseaga sanaa.

Na AMBILE BERNARD, MRATIBU PESD, BJL

Okay tuanze na Mithali 28:13

Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema.
—Mithali 28: 13 (Biblia Takatifu)

Biblia inasema… bali yeye aziungamae na kuziacha atapata rehema

Kuna maneno mawili pale;
1. Aziungamae
2. Atapata rehema

Kuungamana ni nin??

Kuungama ni sawa na kusema kukiri au kukubali. Kwa kiingereza wanasema comfess.

Kuungama ni kukiri na kukubali kwa kinywa chako makosa yako uliyofanya. Kuungama sio kutubu, hivi ni vitu viwili tofauti kabisa.

Unaweza ukaungama leo, kesho ukarudia kosa lile lile ulilokiri jana.

Twende na Yeremia 8:6

Nalisikiliza nikasikia, lakini walisema yasiyo sawa; hapana mtu aliyetubia maovu yake, akisema, Nimefanya nini? Kila mtu hurudia mwendo wake mwenyewe, kama farasi aendavyo kasi vitani.
—Yeremia 8: 6 (Biblia Takatifu)

Kuungama ni process ya kuelekea toba halisi. Biblia inasema hakuna alietubia maovu yake yani hakuna mtu ambae aliungama na matokeo yake kila mtu aliendelea na maovu yake.

Mungu anasema alisikiliza akaskia dooh! kuna lugha mbili hapa; aliskiliza halaf akaskia.

Naam yanatafsiri hivi kwasababu ukisoma mbele utaona anasema KILA MTU HURUDIA MWENDO WAKE MWENYEWE, ina maana watu hawa walikuwa hawatubu ila wanaungama.

Kurudia mwendo maana yake wanakubali halafu hawaachi makosa yao. Lakin Mungu anasema aliskiliza then akaskia. So kumbe kuna tofauti kati ya kuskiliza na kuskia; maana anasema walisema yasio sawa.

Yasio sawa Ndo yapi hayo?

Unapoungama acha usanii sababu Mungu anaupeleleza moyo wako. Unajua kila kitu kuhusu wewe. Sasa unapoungama sema kweli kubali makosa yako sio unaanza visingizio mara hivi mara vile mara ooh… asingekuwa mke wangu nisingetukana au nisingempiga… Mungu hakuelewi.

Kuskiliza ni nje (masikioni), kuskia ni ndani (moyoni)

Huwezi kuskiliza halafu ukatenda mapenzi ya Munguz, haiwezekani, ila unaweza ukatenda mapenzi ya Mungu kwasababu umeskia.

Kuskia kwa maana nyingine katika kutenda mapenzi ya Mungu in kutii.

Itakuwa utakaposikia sauti ya Bwana, Mungu wako, kwa bidii, kutunza kuyafanya maagizo yake yote nikuagizayo leo, ndipo Bwana, Mungu wako, atakapokutukuza juu ya mataifa yote ya duniani;
—Kumbukumbu la Torati 28: 1 (Biblia Takatifu)

Hapa kwanin hajatumia kuskiliza ila kasema kuskia… Biblia ya kiingereza inasemaje hapa? Biblia ya kiingereza inasema OBEY. Kwa maana nyingine naweza kusema utakapotii sauti ya Mungu…

Turudi huku, Mungu alisikiliza lakini alipokuwa anaskia akaona hawa jamaa hawapo serious hawamaanishi wanachotamka.

Wamekosa utii kabisa ndani ya mioyo yao.

Na ukikosa utii huwezi maanisha chochote. Ndipo akasema hakuna alietubia uovu wake yaani wote walikuwa wanaruka ruka tuu hawamaanishi.

Sasa uthibitisho wa kuwa walikuwa hawamaanishi ni pale walikuwa wanarudia miendo yao kama farasi.

Unakiri leo kesho unarudia…

Unajua kwanini unarudia? …kwasababu hujatubu bado.

Sasa ngoja nikuoneshe toba ni nini? Turudi kwenye Mithali 28:13

Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema.
—Mithali 28: 13 (Biblia Takatifu)

Kwanza ijulikane wazi ukificha dhambi zako sawasawa na Yeremia 8:6 hutafanikiwa. Sasa hapa akasema …bali yeye aziungamae yan anaekiri halafu akasema na “kuziacha.”

Kumbe kukiri sio kuacha… kukiri ni kukubali tu kwa kinywa chako, haina maana ndo umeacha.

Sasa kumbe kuacha ndo kupi??? ….kuacha maana yake ndo TOBA!

Toba ni nini??

Toba ni kugeuka …toba haipo kimaneno, toba ipo kivitendo, …toba maana yake kuacha! Yaani kama ulikuwa unaelekea kusini then unageuka unaelekea kaskazini hiyo ndo maana ya toba.

Sijagusa kabisa rehema! …nazungumzia toba sasa.

Naomba hapa niweke sawa maana hapa huwa tunachanganya sana tunajikuta tunaomba toba kila siku hata Mungu anatushangaa.

Toba ni mara moja tuu pale ulipoamua kukata shauri na kuamini kazi ya msalaba, biashara ya toba iliishia pale ooh unaweza ukajiuliza sasa hii tunayofanyaga au unayofanyaga kila siku inaitwa nini?

Sikiliza; ulipookolewa kwa neema kupitia Kristo Yesu dhambi zako zote zilifutwa ukahamishwa ulimwengu kutoka ulimwengu wa giza kwenda ulimwengu wa nuru. Huku ndo kugeuka, kuacha dhambi, uovu na makosa.

Biblia inasema aliezaliwa na Mungu hatendi dhambi; sasa wewe kila siku huwa unatubu nini mpendwa wakati ulishahamishwa ulimwengu!

Toba siyo kuomba msamaha. Ukikosea lazima uombe msamaha na msamaha haombwi Mungu tuu hata mwanadamu mwenzio anaombwa msamaha mradi umemkosea.

Ukishahamishwa ulimwengu, Mungu hakuoni wewe anamuona Kristo. Ukishakuwa katika ulimwengu wa mwana wa pendo lake Mungu anamuona Kristo sio wewe tena.

Maana Biblia inasema yeye yupo ndani yetu na sisi ndani yake. Tuliza akili hapa kwenye toba usikosee tena!

Ukishaokoka unahesabiwa haki hapo hapo. Mungu hakuoni tena mwenye hatia mbele zake.

Hata kama ulishaua maelfu ya watu ukishaokoka unahesabiwa haki tena buree bila gharama yoyote maana mwanae mpendwa alishalipa gharama.

Toba ni kugeukia ulimwengu wa mwana wa pendo lake, biashara inaishia hapo. Huko kutubu unakotubu kila siku unatubu nini mpendwa??

Ntakuelewesha unachotakiwa kufanya,

Sikia, siyo kwamba Mungu hajui madhaifu yako lakini unajua Mungu anasemaje kuhusu udhaifu wako?

Mungu anasema yeye hujitukuza kupitia udhaifu. Paulo alikuwa na mwiba ambao alimuomba Mungu autoe lakini Mungu alimkatalia na kumwambia neema yangu yatosha sijui kama naeleweka hapa.

Anajua udhaifu wako lakini pamoja na kujua udhaifu wako hutakiwi kabisa kufanya dhambi maana wewe siyo wa ulimwengu huu!

Ngoja nikupe kisa cha Isaya yamkini utanielewa.

Ukisoma ile Isaya kuanzia sura ya kwanza hadi ya tano; Isaya alikuwa anafanya huduma na alikuwa anatumika sanaa. Lakini pamoja na kutumika kwake uovu ulikaa ndani yake bila hata yeye kujua kuwa kuna uovu umetulia ndani yake kimya kabisaa.

Sasa unajua kwanini Isaya hakujua???

Isaya hakujua kwa sababu ya neema ya Mungu iliokuwepo juu yake. Lakini badae alikuja kujua. Alijuaje???

Ukisoma kuanzia ile sura ya sita utagundua Isaya aligundua uovu uliopo ndani yake. Kwanini? …kwasababu Mungu aliiondoa neema yake iliokuwa juu ya Isaya then akabaki Isaya kama Isaya, pale ndo alipojua kuwa yeye ni muovu.

Aliiondoa, alitaka tu kumuonesha kuwa pamoja kwamba unatumika lakini kuna kitu hakipo sawa kwako na hakionekani sababu ya neema yangu.

Isaya akajua kuwa ana kinywa kilichojaa uovu kinywa kilichojaa matusi. Biblia inasema malaika akaweka kaa la moto kwenye kinywa cha Isaya na uovu ukamtoka.

Sasa Agano Jipya si zaidi ya Agano la kale???sikiliza, Mungu hakuoni wewe mwenye hatia ulishatubu kwa kuhamishwa ulimwengu, acha kufanya toba kila siku hata Mungu anakushangaa alishakusamehe kipindi ulijua kazi ya msalaba.

Sasa unaweza ukajiuliza ufanyeje sasa ukikosea???

Hii notion ya kukosea siipendagi saanaa kuitumia sababu inahalalisha watu wakosee wakijua kuwa watasamehewa. Wewe umezaliwa na Mungu hutendi dhambi sasa hizo dhambi unazofanya na kutubu kila siku ni zipi mpendwa???

Sijahama kwenye toba… mind you toba siyo msamaha.

Udhaifu wako unafichwa na Kristo maana Mungu hakuoni wewe tena bali anamuona Kristo. Acha kutaka kuhalalisha udhaifu wako kusema kuwa ndo unakurudisha nyuma.

Hivi mnajua maana kuketishwa pamoja na Kristo???

Yaani kula yako, ongea yako, vaa yako, harufu yako, kila kitu chako ni Kristo; hadi DNA yako ni Kristo haya huko kutubu kwa kila siku kunatoka wapi??

Alipoketi yeye na wewe uko hapo, sasa yeye akinukia na wewe si utanukia harufu kama yake? Kwani Yesu tunamchukuliaje?

Toba ni only once in a period of a humankind life…

Sasa tuje kuangalia rehema.

Biblia inasema bali aungamae na kuziacha atapata rehema.

Rehema ni nini?

Rehema ni msamaha ambao mtu hastahili kuupata, na hapa wapendwa wengi tunachanganya na toba.

Unaomba rehema unasema toba. Yaani mtu ukiangalia maisha yako unaona kabisa hustahili hata kuishi lakini rehema ya Mungu inakufanya uishi.

Hivi ukifanya dhambi makusudi unastahili kuomba nini toba au rehema????

Unatakiwa kuomba rehema na sio TOBA. Unaomba kusamehewa kosa ambalo hustahili kusamehewa.

Ndo maana Biblia inasema aungamae na kuziacha atapata rehema, yaani anaekiri na kugeuka sawasawa na Warumi 10:9-10 atapata rehema yaani atapata msamaha.

Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu.
—Warumi 10: 9-10 (Biblia Takatifu)

Unapogundua umekosea wapaswa kuomba rehema kwa maana ya msamaha na siyo toba.

Walokole wengi tunakwama hapa!

Utakaso ni nini?

Hebu tuone Isaya 1:18

Haya, njoni, tusemezane, asema Bwana. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu.
—Isaya 1: 18 (Biblia Takatifu)

Huu ndo utakaso. Utakaso ni kwa ajili ya ondoleo la dhambi na kinachotakasa ni damu ya Yesu Kristo pekee.

Damu ya Yesu ni kwa ajili ya utakaso na hii kazi ilishamilizika Yesu alipokufa msalabani. Jamani unapokuwa ndani ya ufalme wewe sio mtu wa kawaida tena.

Shida ni kwamba tunashindwa kumdhihirisha Kristo kimatendo ila Kristo yuko ndani yetu kinadharia ndo maana kila siku tunataka utakaso.

Kuna watu wanaweza wasinielewe hapa lakini muda wa kujadili dhambi umekwisha ni wakati wa kujua na kutenda mapenzi ya Mungu.

Tunampa shetani milleage isiyokuwa na maana yoyote. Ulishatakaswa tayari unataka utakaso upiii??

Hivi mmesoma sala na maombi ya Paulo? kuna mahali popote aliomba utakaso? Ukipata muda soma maombi ya Paulo kuna kitu cha kujifunza hata maombi ya Yesu kuna mahali alikuwa anawaombea wanafunzi wake hakuna sehemu aliomba toba wala utakaso.

Tunarudia mambo ambayo Yesu alishayafanya tayari.

Kuna muda tunajibebesha mizigo isiyo na maana wala isiyotuhusu.

(Kutoka katika program yetu ya MASWALI NA MAJIBU kwenye group la WhatsApp kila jumamosi)