Na; Edna Kwayu

Neno la kusimamia tunasoma katika kitabu cha Mwanzo 39:21 Biblia nakala ya SUV; “Mungu anataka kutuonyesha umuhimu wa kutembea na kibali chake ili kufikia kwenye hatma yako”

Nguvu ya kibali cha Bwana katika maisha yako

Lakini BWANA akawa pamoja na Yusufu, akamfadhili, akampa kibali machoni pa mkuu wa gereza.

Tunasoma pia katika kitabu cha Esta 5:2 nakala ya SUV, Biblia inasema, “Mungu anataka kutuonyesha nguvu za kibali chake kwenye maisha yetu”

Ikawa, mfalme alipomwona malkia Esta amesimama uani, yeye akapata kibali machoni pake; naye mfalme akamnyoshea Esta fimbo ya dhahabu aliyokuwa nayo mkononi. Basi Esta akakaribia, akaigusa ncha ya fimbo.

Tuanze somo letu…

Kibali ni nini?

Kibali ni hali ya kukubalika kufanya jambo au kufanya kitu Fulani. Kibali ni kupokelewa kwa watu, Mungu. Mfano mzuri Habili  alitakabaliwa/alipata kibali kwa sadaka yake. Maana nyingne ya kibali ni kupewa nafasi kwenye moyo wa mtu/mioyo ya watu. Soma katika andiko hili la 2 Wakorintho 7:2, Biblia inasema, “Tupeni nafasi mioyoni mwenu. Hatukumdhulumu mtu ye yote, wala kumharibu mtu, wala kumkaramkia mtu.”

Kibali ni kitu cha kiroho kwanza kabla hakijaonekana kwa jinsi ya mwili. Kibali halisi lazima kitoke kwa Mungu mwenyewe na kisichotoka kwa Mungu hakidumu. Kuna nguvu na maisha zaidi pale unapopata kibali kwa Mungu kwanza, ndipo akupe kibali machoni pa watu.

Kinachotangulia kabla ya kibali ni Neema. Tuangalie kwenye neno hili, Wagalatia 2:9, Biblia inasema, “tena walipokwisha kuijua ile neema niliyopewa; Yakobo, na Kefa, na Yohana, wenye sifa kuwa ni nguzo, walinipa mimi na Barnaba mkono wa kuume wa shirika; ili sisi tuende kwa Mataifa, na wao waende kwa watu wa tohara”

Neema hutangulia ndipo kibali hufuatilia. Unapoona una karama ya uimbaji tambua Mungu alikupa Neema kisha akaachia karama ndani, hivyo karama na Neema hufanya kazi Pamoja. Unapoona unafanya jambo fulani na linaenda vizuri ujue Neema ya Mungu ilitangulia. Ipo nguvu kubwa sana kwenye kibali cha Bwana katika maisha yako. Neema unapewa bure kwa imani lakini ukifanya vema utapata kibali.

Tusome katika Mwanzo 37:3-5.

“Basi Israeli akampenda Yusufu kuliko wanawe wote, maana ni mwana wa uzee wake, akamfanyia kanzu ndefu. Ndugu zake wakaona ya kuwa baba yao anampenda kuliko ndugu zake wote, wakamchukia, wala hawakuweza kusema naye kwa amani. Yusufu akaota ndoto, akawapa ndugu zake habari, nao wakazidi kumchukia”

Unaona? kibali kina vita ndani yake.

Katika 1 Samweli 2:26, Biblia inasema hivi; “Na yule mtoto, Samweli, akazidi kukua akapata kibali kwa BWANA, na kwa watu pia.”

Kabla ya kufanya jambo tafuta kibali cha Bwana kwanza. Samweli alipata kibali machoni mwa Bwana na watu kabla ya kuanza huduma yake.

Kibali cha Bwana kina gharama yake na kinatunzwa. Kinahitaji matunzo na ili utambue au kutunza kibali inatakiwa kuitunza Neema iliyokupa kibali

Waebrania 12:15, “mkiangalia sana mtu asiipungukie neema ya Mungu; shina la uchungu lisije likachipuka na kuwasumbua, na watu wengi wakatiwa unajisi kwa hilo.”

Gharama ya kutunza kibali.

  • utakatifu.
  • Uaminifu
  • Unyenyekevu
  • Maombi

Danieli 6:4, “Basi mawaziri na maamiri wakatafuta sana kupata sababu za kumshitaki Danieli kwa habari za mambo ya ufalme; lakini hawakuweza kuona sababu wala kosa; kwa maana alikuwa mwaminifu, wala halikuonekana kosa wala hatia ndani yake.”

1 Petro 5:5-6; “Vivyo hivyo ninyi vijana, watiini wazee. Naam, ninyi nyote jifungeni unyenyekevu, mpate kuhudumiana; kwa sababu Mungu huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa wanyenyekevu neema. Basi nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake”

Kunyenyekea ni kujifanya hujui ili kuongeza zaidi na kukubali kila akifanyacho mwenzio. Ni kujifanya hujui ili kufikia lengo. Watumishi leo tumekua wajuaji sana yaani unajikuta we ndio unajua sana biblia kuliko mwenzio. Kama utakua mnyenyekevu na kujifanya hujui basi tutajua mengi sana na Mungu atatuinua

Fanya maombi kuwa ni mfumo wako wa kila siku jengea mazoea maisha ya kawaida. Omba asubuhi, mchana na jioni.

Kibali huja na majukumu. Mungu hawezi kukupa kibali bure anakupa na kazi ya kufanya. Usipotimiza jukumu lake atakiondoa kibali.

KIBALI CHA ESTA

  1. Mungu alimpa kibali chake kilichompa kibali mbele za watu waliomwona na mbele za mfalme.

Esta 2:15.

15. Hata ilipowadia zamu yake Esta, binti Abihaili, mjomba wake Mordekai, ambaye alimtwaa kuwa binti yake, ili aingie kwa mfalme, yeye hakutaka kitu, ila vile vilivyoagizwa na Hegai, msimamizi wake mfalme, mwenye kuwalinda wanawake. Naye huyu Esta alikuwa amepata kibali machoni pa wote waliomwona.

  • Kibali cha Esta kilikua na kazi ya kufanya hakikuja bure.

Esta 4:14.

14. Kwa maana wewe ukinyamaza kabisa wakati huu, ndipo kutakapowatokea Wayahudi msaada na wokovu kwa njia nyingine; ila wewe utaangamia pamoja na mlango wote wa baba yako; walakini ni nani ajuaye kama wewe hukuujia ufalme kwa ajili ya wakati kama huo?

Jukumu alilipewa Esta ni kupangua waraka wa hamani na kuwakomboa wayaudi na mauti.

  • Wakati wa kibali cha Esta kutimiza jukumu lake vita ya kibali iliinuka.

Esta 4:11.

11. Watumwa wote wa mfalme wanajua sana, hata na watu wa majimbo ya mfalme, ya kwamba mtu ye yote, akiwa mwanamume au mwanamke, atakayemjia mfalme katika ua wa ndani, wala hakuitwa, kuna sheria moja kwake, ni kwamba auawe; isipokuwa yeye ambaye mfalme atamnyoshea fimbo ya dhahabu, ili aishi; wala mimi sikuitwa niingie kwa mfalme yapata siku thelathini.

Vita ya kibali haiinuki wakati wowote, huinuka wakati wa kuanza kutimiza jukumu.

  • Kibali cha Esta kiliachilia hekima na mbinu ya kutekeleza mbinu za kibali.

KIBALI CHA YUSUFU

  1. Mungu alimpa Yusufu kibali na akapata kibali mbele ya baba yake kuliko watoto wengine wote.

Alipata kibali kwa kila aliyekua anamuona.

Mwanzo 37:3.

3. Basi Israeli akampenda Yusufu kuliko wanawe wote, maana ni mwana wa uzee wake, akamfanyia kanzu ndefu.

  • Kibali cha Yusufu kilikua na kazi, kilikua kimebeba haya yafuatayo.
  • Kibali cha Yusufu kilikua kimebeba baraka ndani yake.

Mwanzo 39:5.

5. Ikawa tokea wakati alipomweka awe msimamizi juu ya nyumba yake, na vyote vilivyomo, BWANA akabariki nyumba ya yule Mmisri kwa ajili ya Yusufu. Mbaraka wa BWANA ukawa juu ya vyote alivyokuwa navyo katika nyumba, na katika shamba.

– Kibali cha Yusufu kilikua kimebeba uongozi

– Kibali cha Yusufu kilikua kimebeba kumcha Bwana

Mwanzo 39:9.

9. Hakuna mkuu katika nyumba hii kuliko mimi, wala hakunizuilia kitu cho chote ila wewe, kwa kuwa wewe u mkewe. Nifanyeje ubaya huu mkubwa nikamkose Mungu?

– Kibali cha Yusuph kilikua kimebeba hekima ya kufasiri ndoto

Mwanzo 40:9-19.

9. Mnyweshaji mkuu akamhadithia Yusufu ndoto yake; … 12. Yusufu akamwambia, Tafsiri yake ndiyo hii. Matawi matatu ni siku tatu. 13. Baada ya siku tatu Farao atakiinua kichwa chako, atakurudisha katika kazi yako; nawe utampa Farao kikombe mkononi mwake, kama desturi ya kwanza, ulipokuwa mnyweshaji wake … 16. Mkuu wa waokaji alipoona ya kwamba hiyo tafsiri ni ya mema, akamwambia Yusufu, Mimi kadhalika nilikuwa katika ndoto yangu, … 18. Yusufu akajibu, akasema, Tafsiri yake ndiyo hii Nyungo tatu ni siku tatu. 19. Baada ya siku tatu Farao atakiinua na kukuondolea kichwa chako, na kukutundika juu ya mti, na ndege watakula nyama yako.

– Kibali cha Yusuph kilikua kimebeba maisha ya watu wengi ikiwepo ndugu zake kipindi cha njaa.

Mwanzo 45:5-6.

5. Basi sasa, msihuzunike, wala msiudhike nafsi zenu, kwa kuniuza huku; maana Mungu alinipeleka mbele yenu kuhifadhi maisha ya watu. 6. Maana miaka hii miwili njaa imekuwa katika nchi, na iko tena miaka mitano isiyo na kulima wala kuvuna.

– Kibali cha Yusuph kilikua kimebeba elimu ya wakati ujao (jicho linaloona kesho)

  • Gharama ya kibali cha Yusufu kilikua ni utakatifu yaan kujitunza nafsi.

Mwanzo 39:9.

9. Hakuna mkuu katika nyumba hii kuliko mimi, wala hakunizuilia kitu cho chote ila wewe, kwa kuwa wewe u mkewe. Nifanyeje ubaya huu mkubwa nikamkose Mungu?

Matendo ya Mitume 20:28.

28. Jitunzeni nafsi zenu, na lile kundi lote nalo, ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa waangalizi ndani yake, mpate kulilisha kanisa lake Mungu, alilolinunua kwa damu yake mwenyewe.

  • Kibali cha Yusufu kilipata shambulio.

Shambulio la kwanza la kibali cha Yusufu kilikua kwenye familia yake.

Mke wa Potifa alimpiga vita Yusufu

Mwanzo 39:6.,7.,8.,9.,10.,11.,12.,13.,14.,15.,16.,17.,18.,19.,20.,21.

11. Ikawa, siku moja, akaingia nyumbani atende kazi yake, wala hapakuwa na mtu katika watu wa nyumbani humo ndani; 12. huyo mwanamke akamshika nguo zake, akisema, Lala nami. Yusufu akaiacha nguo yake mkononi mwake, akakimbia, akatoka nje. 13. Ikawa alipoona ya kwamba amemwachilia nguo yake mkononi mwake, naye amekimbia nje, 14. akawaita watu wa nyumbani mwake, akasema nao, akinena, Angalieni, ametuletea mtu Mwebrania atufanyie dhihaka. Ameingia kwangu, ili alale nami, nikalia kwa sauti kuu. 15. Ikawa, aliposikia ya kuwa nimepaza sauti yangu na kulia, aliiacha nguo yake kwangu, akakimbia, akatoka nje. 16. Basi akaiweka ile nguo kwake hata bwana wake aje nyumbani. 17. Naye akamwambia kama maneno hayo, … 19. Ikawa bwana wake aliposikia maneno ya mkewe aliyomwambia, akisema, Mtumwa wako amenitendea mambo kama haya, hasira yake ikawaka. 20. Bwana wake akamtwaa Yusufu, akamtia gerezani, mahali walipofungwa wafungwa wa mfalme, naye akawamo humo gerezani. 21. Lakini BWANA akawa pamoja na Yusufu, akamfadhili, akampa kibali machoni pa mkuu wa gereza.

Wakati unapigwa vita juu ya kibali chako Mungu humwinua mtu kwa ajili yako. Kuna shambulizi la kibali linaumiza lakini ndilo linalokupeleka kwenye hatma yako.

Kuna wakati unatakiwa kukushambuliwa ili wakupeleke kwenye hatma yako. Shambulizi la ndugu wa Yusufu lilipelekea Yusufu kufikia kwenye hatma yake. Shambulizi la kibali lilimpeleka Yusufu gerezani.