BIBLIA NI JIBU LAKO

Neno la Mungu na likae kwa wingi ndani yako katika hekima yote

About us

KUHUSU BJL:

BJL(Biblia ni Jibu Lako), ni taasisi ya kidini/Kikristo (FBO) isiyo ya kiserikali (NGO) inayounganisha jamii ya wana wa Mungu (Yoh. 1:14). Msingi wa IMANI yetu ni BIBLIA TAKATIFU ambalo ndiyo NENO LA MUNGU ALIYE HAI.

MOTTO:

“Neno la Mungu na lijae kwa wingi mioyoni mwenu”

DHIMA:

1. Kulijaza Neno la Mungu ndani ya mioyo yetu katika hekima yote kwa kufundishana, kuelekezana na kuonyana.

“Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu.” Wakolosai 3 :16

2. Kulitunza Neno la Mungu vinywani mwetu na kulitafakari kila wakati, mchana na usiku ili tupate kutenda sawasawa na yote yaliyoandikwa katika Biblia.

“Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana.” Yoshua 1 :8

DIRA:

1. Kzidi katika kuwafanya mataifa wanafunzi wa Yesu Kristo.

“Na wale wanafunzi kumi na mmoja wakaenda Galilaya mpaka mlima ule aliowaagiza Yesu. Nao walipomwona, walimsujudia; lakini baadhi yao waliona shaka. Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.” Mathayo 28 :16-20

2. Kutengeneza jamii ya wana wa Mungu waliokamilika katika Neno la Kristo katika kuujenga mwili wa Kristo.

“Kwa kuwa watu wengi wametia mikono kutunga kwa taratibu habari za mambo yale yaliyotimizwa katikati yetu, kama walivyotuhadithia wale waliokuwa mashahidi wenye kuyaona, na watumishi wa lile neno tokea mwanzo, nimeona vema mimi nami, kwa kuwa nimejitafutia usahihi wa mambo hayo yote tangu mwanzo, kukuandikia kwa taratibu, Theofilo mtukufu, upate kujua hakika ya mambo yale uliyofundishwa.” Luka 1 :1-4

MALENGO & MIKAKATI:

1) Kuhubiri INJILI kwa wati wote.
“Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa.” Marko 16 :15-16

2) Kufundisha KWELI na HAKIKA ya Neno la Mungu.
“Watu hawa walikuwa waungwana kuliko wale wa Thesalonike, kwa kuwa walilipokea lile neno kwa uelekevu wa moyo, wakayachunguza maandiko kila siku, waone kwamba mambo hayo ndivyo yalivyo.” Matendo ya Mitume 17 :11

3) Kujibu maswali tete na yenye utata katika WOKOVU kwa namna ya maelekezo ya Neno la Mungu.
“Wapenzi, msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani.” 1 Yohana 4 :1
“jaribuni mambo yote; lishikeni lililo jema;” 1 Wathesalonike 5 :21

4) Kuhamasisha usomaji wa NENO la Mungu na kufanya MAOMBI,
“Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana.” Yoshua 1 :8
“ombeni bila kukoma;” 1 Wathesalonike 5 :17 “Dumuni sana katika kuomba, mkikesha katika kuomba huku na shukrani;” Wakolosai 4 :2

5) Kufanya huduma zingine za INJILI ya UPENDO.
“Mtu akidhani ya kuwa anayo dini, wala hauzuii ulimi wake kwa hatamu, hali akijidanganya moyo wake, dini yake mtu huyo haifai. Dini iliyo safi, isiyo na taka mbele za Mungu Baba ni hii, Kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao, na kujilinda na dunia pasipo mawaa.” Yakobo 1 :26-27

KARIBU SANA NDANI YA BIBLIA NI JIBU LAKO