BIBLIA NI JIBU LAKO
Naitwa Binti (Miss) Huruma Pharles Nyamweru, Ruvuma.

Mawasiliano +255(0)759 981495

UTANGULIZI:
Bwana Yesu Kristo asifiwe sana; nawasalimia katika Jina la Yesu Kristo; Moja kwa Moja tuingie katika somo, yawezekana umeshawahi kulisikia Neno hilo na Somo hilo, Lakini naamini naamini Mungu anamakusudi na kila mmoja katika siku ya leo

Maombi ni nini?

Maombi ni nini? “Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami.” Ufunuo wa Yohana 3:20

Maana ya kwanza Ni kumkaribisha Yesu ndani ya mioyo yetu ili ashukughulike na uhitaji wetu/mahitaji yetu.

Maana nyingine ya Maombi ni silaha ya kuzuia mtu asiingie katika majaribu na pia Ni silaha ya kutegua mitego iliyotegwa na adui bila wewe kujua. “Alipofika mahali pale aliwaambia, Ombeni kwamba msiingie majaribuni Luka 22:40, pia Luka 22:46b inasema, Ondokeni, mkaombe, msije mkaingia Majaribuni.”

Nimeeleza kifupi maana ya maombi nifikie kwenye Somo, nafikiri Umeanza kupata kitu.

HATUA ZA KUFUATA TUNAPOKUWA TUNAFANYA MAOMBI YA KUMUGUSA MUNGU:

I. Hatua ya KWANZA; Kuomba rehema mbele za Mungu; “Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote. 1 Yohana 1:9

II. Hatua ya PILI; Amini kwamba Mungu yupo na huwasikia wale wamuombao; “Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.” Waebrania 11:6. “Kwa sababu hiyo nawaambia, Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu.” Marko 11:24.

III. Hatua ya TATU; Omba kwa kutumia jina la Yesu. Nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana. Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya. Yohana 14:13-14.

IV. Hatua ya NNE; Mahali pa kuombea, Unaweza kuombea mahali popote penye utulivu mfano chumbani au sehemu yoyote iliyo na utulivu; “Bali wewe usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.” Mathayo 6:6

V. Hatua ya TANO; Muda wa kuomba unaweza kujipangia kulingana na muda wako lakini Biblia inasisitiza kiwango cha chini cha Muombaji angalau iwe SAA moja; “Akawajia wale wanafunzi, akawakuta wamelala, akamwambia Petro, Je! Hamkuweza kukesha pamoja nami hata saa moja?” Mathayo 26:40

VI. Hatua ya SITA kusimamia Neno la Mungu (kuomba kwa kutumia Neno la Mungu); “Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa.” Yohana 15:7, “Ndipo Bwana akaniambia, Umeona vema, kwa maana ninaliangalia neno langu, ili nilitimize.” Yeremia 1:12

VII. Hatua ya SABA na ya mwisho kwa maandalizi yangu ni Kushukuru; “Dumuni sana katika kuomba, mkikesha katika kuomba huku na shukrani” Kolosai 4:2. “Namshukuru Mungu, nimwabuduye kwa dhamiri safi tangu zamani za wazee wangu, kama vile nikukumbukavyo wewe daima, katika kuomba kwangu usiku na mchana.” 2 Timotheo 1:3

AINA ZA MAOMBI YANAYOMGUSA MUNGU:

1. Maombi ya Usiku au alfajiri: Haya maombi ukisoma vifungu vifuatavyo vizuri, utagundua ni Maombi yanayofungua vifungo mbalimbali na kumuweka mtu kuwa huru zaidi, naomba mpitie vifungu hivyo, ili maswali yapatikane.

“Yakobo akakaa peke yake; na mtu mmoja akashindana naye mweleka hata alfajiri. Naye alipoona ya kuwa hamshindi, alimgusa panapo uvungu wa paja lake; ukateguka uvungu wa paja la Yakobo alipokuwa akishindana naye. Akasema, Niache, niende, maana kunapambazuka. Akasema, Sikuachi, usiponibariki. Akamwuliza, Jina lako n’nani? Akasema, Yakobo. Akamwambia, Jina lako hutaitwa tena Yakobo, ila Israeli, maana umeshindana na Mungu, na watu, nawe umeshinda.” Mwanzo 32:24-28

“Ikawa siku zile aliondoka akaenda mlimani ili kuomba, akakesha usiku kucha katika kumwomba Mungu.” Luka 6:12

“Hata alfajiri na mapema sana akaondoka, akatoka akaenda zake mahali pasipokuwa na watu, akaomba huko.” Marko 1:35

“Na alipokuwa akifikiri haya akafika nyumbani kwa Mariamu, mamaye Yohana, ambaye jina lake la pili ni Marko; na watu wengi walikuwa wamekutana humo wakiomba.” Matendo ya Mitume 12:12

“Lakini panapo usiku wa manane Paulo na Sila walikuwa wakimwomba Mungu na kumwimbia nyimbo za kumsifu, na wafungwa wengine walikuwa wakiwasikiliza. Ghafula pakawa tetemeko kuu la nchi, hata misingi ya gereza ikatikisika, na mara hiyo milango ikafunguka, vifungo vya wote vikalegezwa.” Matendo ya Mitume 16:25-26

2. Maombi ya kufunga: Haya Maombi yanaleta majibu haraka kuliko tunavyofikiri, mara nyingi hutupa Neema na kibari Mahali ambapo hatustahili kupata uhitaji wetu, na pia ni Maombi yanayotuepusha na majaribu mbalimbali katika maisha yetu ya kila siku. Somo maandiko hapa chini.

“Naye alikuwa huko pamoja na Bwana siku arobaini na masiku yake; hakula chakula, wala hakunywa maji. Naye akaandika katika hizo mbao, hayo maneno ya maagano, hizo amri kumi.” Kutoka 34:28

“Ikawa baadaye, wana wa Moabu, na wana wa Amoni, na pamoja nao baadhi ya Wameuni, wakaja juu ya Yehoshafati vitani. Wakaja watu waliomwambia Yehoshafati, wakisema, Wanakuja jamii kubwa juu yako watokao Shamu toka ng’ambo ya bahari; na tazama, wako katika Hasason-tamari (ndio En-gedi). Yehoshafati akaogopa, akauelekeza uso wake amtafute Bwana; akatangaza mbiu ya watu kufunga katika Yuda yote. Yuda wakakusanyika pamoja ili wamtafute Bwana; hata kutoka miji yote ya Yuda wakaja kumtafuta Bwana.” 2 Mambo ya Nyakati 20:1-4

“Uende ukawakusanye Wayahudi wote waliopo hapa Shushani, mkafunge kwa ajili yangu; msile wala kunywa muda wa siku tatu, usiku wala mchana, nami na wajakazi wangu tutafunga vile vile; kisha nitaingia kwa mfalme, kinyume cha sheria; nami nikiangamia, na niangamie. Basi Mordekai akaenda zake, akafanya yote kama vile Esta alivyomwagiza.” Esta 4:16-17

“katika mwaka wa kwanza wa kumiliki kwake, mimi Danielii, kwa kuvisoma vitabu, nalifahamu hesabu ya miaka, ambayo neno la Bwana lilimjia Yeremia nabii, ya kuutimiza ukiwa wa Yerusalemu, yaani, miaka sabini. Nikamwelekezea Bwana Mungu uso wangu, ili kutaka kwa maombi, na dua, pamoja na kufunga, na kuvaa nguo za magunia na majivu.” Danieli 9:2-3

“Kisha Yesu alipandishwa na Roho nyikani, ili ajaribiwe na Ibilisi. Akafunga siku arobaini mchana na usiku, mwisho akaona njaa.” Mathayo 4:1-2

“Palikuwa na nabii mke, jina lake Ana, binti Fanueli, wa kabila ya Asheri, na umri wake ulikuwa miaka mingi, alikuwa amekaa na mume miaka saba baada ya uanawali wake. Naye ni mjane wa miaka themanini na minne; haondoki katika hekalu, ila huabudu usiku na mchana kwa kufunga na kuomba.” Luka 2:36-37

3. Maombi ya kutumia Neno la Mungu: Kwa kutumia Neno la Mungu, katika maombi, Mungu hushuka na hutujibu maombi yetu, nami nilipotumia Neno la Mungu katika maombi yangu nimemuona Bwana kupita maelezo, wala Mungu hakunipita kwa jambo lolote.

“Ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu; halitanirudia bure, bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma.” Isaya 55:11

“Maana Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo. Wala hakuna kiumbe kisichokuwa wazi mbele zake, lakini vitu vyote vi utupu na kufunuliwa machoni pake yeye aliye na mambo yetu.” Waebrania 4:12-13

“Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu. Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika.” Yohana 1:1-3

“Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia.” 1 Yohana 5:14

“Ndipo Bwana akaniambia, Umeona vema, kwa maana ninaliangalia neno langu, ili nilitimize.” Yeremia 1:12

4. Maombi ya Nadhiri: Yona 2;9-10 Kupitia Maombi haya Hana alimuona, Mungu. Yona katika tumbo la Samaki alimuona, Mungu Nami Nimemuona Mungu sana katika Maombi haya.

“Ndipo Hana akainuka, walipokwisha kula na kunywa huko Shilo. Naye Eli, kuhani, alikuwa akiketi kitini pake penye mwimo wa hekalu la Bwana. Naye huyo mwanamke alikuwa na uchungu rohoni mwake, akamwomba Bwana akalia sana. Akaweka nadhiri, akasema, Ee Bwana wa majeshi, ikiwa wewe utaliangalia teso la mjakazi wako, na kunikumbuka, wala usinisahau mimi mjakazi wako, na kunipa mimi mjakazi wako mtoto mume, ndipo mimi nitakapompa Bwana huyo mtoto siku zote za maisha yake, wala wembe hautamfikilia kichwani kamwe.” 1 Samweli 1:9-11

“Yakobo akaweka nadhiri akisema, Mungu akiwa pamoja nami, akinilinda katika njia niiendeayo, na kunipa chakula nile, na nguo nivae; nami nikirudi kwa amani nyumbani kwa baba yangu, ndipo Bwana atakuwa Mungu wangu. Na jiwe hili nililolisimamisha kama nguzo litakuwa nyumba ya Mungu; na katika kila utakalonipa hakika nitakutolea wewe sehemu ya kumi.” Mwanzo 28:20-22

5. Maombi ya Shukrani: Haya tena ni maombi ambayo nikiboko kwani Yesu alipoomba aliweza kuwalisha watu elfu tano kwa samaki wawili na mikate mitano haikuwa kawaida. Hii ni kwasababu ya nguvu ya maombi ya shukrani. Soma maandiko hapa chini ujifunze zaidi.

“Namshukuru Mungu wangu siku zote, nikikukumbuka katika maombi yangu.” Filemoni 1:4

“Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye.” Wakolosai 3:17

“Basi wakaliondoa lile jiwe. Yesu akainua macho yake juu, akasema, Baba, nakushukuru kwa kuwa umenisikia. Nami nalijua ya kuwa wewe wanisikia sikuzote; lakini kwa ajili ya mkutano huu wanaohudhuria nalisema haya, ili wapate kusadiki kwamba ndiwe uliyenituma. Naye akiisha kusema hayo, akalia kwa sauti kuu, Lazaro, njoo huku nje. Akatoka nje yule aliyekufa, amefungwa sanda miguuni na mikononi, na uso wake amefungwa leso. Naye Yesu akawaambia, Mfungueni, mkamwache aende zake.” Yohana 11:41-44

“Na amani ya Kristo iamue mioyoni mwenu; ndiyo mliyoitiwa katika mwili mmoja; tena iweni watu wa shukrani.” Wakolosai 3:15

“Namshukuru Mungu wangu kila niwakumbukapo, sikuzote kila niwaombeapo ninyi nyote nikisema sala zangu kwa furaha,” Wafilipi 1:3-4

“Kwa sababu hiyo nimepatikana na mateso haya, wala sitahayari; kwa maana namjua yeye niliyemwamini, na kusadiki ya kwamba aweza kukilinda kile nilichokiweka amana kwake hata siku ile.” 2 Timotheo 1:12

“Nami namshukuru Kristo Yesu Bwana wetu, aliyenitia nguvu kwa sababu aliniona kuwa mwaminifu, akaniweka katika utumishi wake;” 1 Timotheo 1:12

“Kwanza namshukuru Mungu wangu katika Yesu Kristo kwa ajili yenu nyote, kwa kuwa imani yenu inahubiriwa katika dunia nzima.” Warumi 1:8

MASWALI YATOKANAYO NA SOMO:

Swali la KWANZA; anauliza Dada Phoibe BJL

Kuhusu eneo la maombi. Tumeona biblia inasema ukiomba basi uingie chumbani. Sasa je nikiwa kazini sehemu ambayo siwezi pata eneo la utulivu siwezi kuonba huku nikiwa naendelea na majukumu?

MAJIBU; Unaweza ukaomba haujazuiliwa, na Mungu ni mwingi wa Neema aweza kukusikia na kukupatia majibu, Lakini ili Mungu ashukuke na kusema na wewe lazima uwe sehemu tulivu, ndipo Mungu anashuka na kushughulikika na mahitaji Yako twaweza kuona mfano kwa Yesu Mara nyingi alienda kuomba Mlimani Matt. 6:12, Naomba usome

NYONGEZA; Ameeen! Biblia inasema “ombeni bila kukoma” maana yake wakati wowote, mahala popote, iwe unafanya chochote; yaani hata usingizini “unapaswa kutokuacha kuomba” unatakiwa ndani ya moyo wako uendelee kusema maneno na Mungu, yaani kiroho uwe connected na Mungu. Kinachofanya kazi ni mwili na siyo roho, kwa hiyo unauacha moyo wako uendelee kukaa na Mungu katika maombi na huku unatembea, unakula, unalala, unavuna, unaandika nk nk

Swali la PILI; anauliza Hosea Gambo BJL

Maombi ya NADHIRI ni maombi ya namna gani??? Ninapofanya maombi haya napaswa kuzingatia mambo gani???

MAJIBU;

I. Ni maombi ambayo mtu anaahidi kufanya jambo fulani kwa ajiri ya hitaji lake endapo Mungu Atafanya kama alivyoomba ukisoma 1Samweli1:28 Utakutana na habari za Mwanamke aliyekuwa tasa, Alimulilia Bwana akamwambia endapo utafungua tumbo langu ndipo nitakapokutolea mtoto huyo ili akutumikie siku zote za maisha yake, na Mungu akamukumbuka akapata uzao na baada ya hapo, akamtoa huyo mtoto kama alivyoahidi ili awe mtumishi wa Mungu.

II. Mambo ya kuzingatia hapa hasa nikujitakasa MTU anapotaka kuomba maombi haya, pia hatua zote za kuingia kwenye Maombi ya kumgusa Mungu zinahitajika kama utaweza kujifuata na zaidi ya Yote baada ya kujitakasa ni kufuata uongozi wa Roho Mtakatifu Maana yeye ni MWalimu kwa kila jambo, na kadhalika hutuombea kiasi ya kuugua, kusikoweza kuneneka!!! Jambo linguine la msingi sana ni kuitunza nadhiri na kuipeleka, ukishaweka kitu kuwa nadhiri maana yake ni kitakatifu, ni wakfu kwaajili ya Bwana, siyo chako tena.

Swali la TATU; anauliza Felix BJL kutoka Malawi.

A) Maombi ya kufunga ya namna gani yana nguvu kati ya kufunga bila kula na kunywa kitu muda kadha na kufunga unakula jioni?

B) Kuna watu wanafunga kama siku 40 wakisema kama wanaitwa Watawa je mafungo hayo niya kibiblia?

MAJIBU;

A) Ninachokifahamu Maombi ya kufunga Bila kula yana Nguvu sana Mfano Tusome Esta 4:16:17, sura ya 5, 6, 7, Utaona vizuri namna Maombi haya yalivyogeuza Mambo badala ya Wana wa islaili kuuwawa akauwawa adui yao hamani, na Pia tukiangalia mfano kwa Bwana Yesu alipoingia katika Maombi ya kufunga, Aliweza kushinda majaribubMathayo 4:1-11 Inatoa ufafanuzi vizuri, Nikwambie tu haya Maombi ukiweza ni kiboko zaidi ya Kiboko, ukiomba Maombi ya kufunga na kuomba bila kula Mara kwa Mara Unakuwa karibu na Mungu, Mara nyingi unaweza kupata mafunuo, maono n.k

B) Mimi hapa katika swala la kufunga siwezi kumpangia MTU afunge siku ngapi, makini kwa kadiri, Roho wa Mungu anavyomjalia mtu afanye hivo hivo, ili Mapenzi ya Mungu aliyejuu yatimie, Kibiblia mtu akiweza inaruhusiwa, Maana tunaona hata Yesu alifunga siku arobani Mathayo 4:1-2, lakini zaidi ya yote nasema mtu afanye kila kitu kwa kadiri Roho wa Mungu anavyomuwezesha maana ukisoma Waefeso 3:20 Biblia inasema atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya Nguvu itendayo kazi ndani yetu, nasisitiza mtu afunge maombi kwa kadiri ya Nguvu itendayo kazi ndani yake na wala sio kufatisha namna wa watu wengine, ijulikane kuwa tunatofautiana nguvu za kiroho.

NYONGEZA; Tunaona kwa Esta anawapa maelekezo akina Modekai, tena kwa msisitizo mkubwa “msile chochote wala msinywe chochote kwa siku zote tatu” ndipo ataweza “kuingia malangoni pa mfalme (behewani)” maana yake haya maombi yakiwa yanafanyika huku mwili umepuuzwa, roho inakuwa active yanakuwa na nguvu isiyo ya kawaida. Yaani mwili unachoka lakini roho inapokea nguvu kubwa sana!

Swali la NNE; anauliza Mwl. Erick BJL

Katika somo lililofindishwa. Je MAOMBI ya kumgusa Mungu sadaka hahitajiki?

MAJIBU;

Nayo pia inaruhusiwa, Sadaka. Siyo lazima kuomba Maombi ya Nadhiri tu, Sadaka inahitajika sana katika Maombi ili Mungu atutakabari, haleluya!! nimegusa kwa sehemu sijagusa kila sehemu, Habari za mfalme Suleman zinanibariki sana alipomtolea Mungu Sadaka Ndipo Mungu akampa kibali juu ya Ufalme na Utawala wake.

Naomba aliyeuliza swali asome 1Nyakati 29:1-25 hakika habari hizi za Mfalme Sulemani zinanibariki sana, na pia soma Mwanzo 8:18-22, na pia soma Mwanzo9;1-17 Baada ya Mtumishi wake Nuhu kutoa Sadaka MUNGU alifurahi sana, hadi akasema atowaangamiza tena watu kwa gharika na akatoa agano la Upinde wa Mungu, mwenyewe. Hakika Neno la Mungu ni pana nalo linanibariki sana, katika kila hali. AMINA!

MUNGU AWABARIKI SANA!