Na; Mathias Elias.


Maombi ni mawasiliano baina ya pande mbili.

Maombi kwa MUNGU” yaani kumwomba Mungu ni mawasiliano baina ya mwanadamu na Mungu ambayo huimarika katika majawabu yatokayo kwa Mungu.

Lengo la somo hili ni kuhimarisha mawasiliano yako na Mungu katika maombi.

Katika somo hili tutaenda na Yakobo 1:5-7

Yakobo 1:5-7; “Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa. Ila na aombe kwa imani, pasipo shaka yo yote; maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari lililochukuliwa na upepo, na kupeperushwa huku na huku. Maana mtu kama yule asidhani ya kuwa atapokea kitu kwa Bwana.”

Pia maombi ni mhimu sana yaambatane na imani maombi yoyote yale yasipokuwa na imani ni sawa na bure. Maombi ya imani ni yale yasiyo kuwa na shaka ndani yake. Sio shaka tu bali shaka ya aina yoyote maana ukiomba kwa shaka kamwe hauta pokea kwa Bwana.

Waebrania 11:1; “Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.”

Na kumbuka kwamba maana ya uhakika ni kutokuwa na mashaka au wasiwasi wa aina yeyote ile. Na uhakika unakuthibitishia ya kwamba kile unacho kiomba au kitarajia ni lazaima kipo au kinakuja.

Ukiwa na mashaka katika maombi tambua moja kwa moja ya kuwa hauna imaani. Na kama hauna imani usitegemee kupokea majibu kutoka kwa Bwana maana Bwana huwajibu wale wanao mwamini katika maombia yao.

Ndiyo ni kanuni yake mwenyewe Mungu wetu.

Mungu anafanya kazi yake kwa kanuni na kama unataka kuishi maisha anayotaka lazima ukubaliane nazo.

Uombapo usiombe kwa mashaka maana mashaka ni kama wimbi

Na sifa ya Wimbi ni kufuata mwelekeo a upepo unako elekea hivyo kama upepo ukivuma kutoka kaskazini kwenda mashariki wimbi hufuata na kama upepo ukigeuza kutoka kaskazini kwenda kusini wimbi nalo hufuata ndivyo alivyo mtu wa mashaka.

Kwahiyo mtu wa tabia kama hizi katika maombi asidhani ya kuwa atapokea kwa Bwana.

…oooh Bwana Yesu asifiweee…

Maombi yenye imani pasipo mashaka ni kama kutembea huku ukienda sehemu unayo ifahamu

kwa mfano mtu anaye tembea kwenda kwao anapo pafahamu uwe na uhakika hawezi kupotea hata siku moja hii ni kwa sabau anafahamu anapo kwenda.

Ndivyo yalivyo na mambi yasio na shaka kwa kuwa humfanya mtu atembee huku akitegemea kupokea kile alicho kiomba kwa Bwana.

Unatakiwa uombe kwa imani pasipo mashaka maana mashaka mashaka yatakufanya usipokee.

Mimi sijui ni wakristo wa ngapi ambao huandika maombi yao huku waki yawekea vema kwa yale yanayo jibiwa ila ninacho kifahamu ni kwamba wengi huwa wanaomba juujuu tu huku wakizani ya kuwa Mungu amesha wajibu kumbe bado wanaishia pasipo kuona matokeo ya kile wanacho kiombea na hii nikutokana na kutokuamini kwao.

Nasema kwa sababu ya kutokuwa na imani kwa sababu kama wangeomba kwa imani nilazima wangepokea kutoka kwa Bwana.

Kumbuka si kuomba tu kwa ajili ya mapepo na wachawi bali Biblia katika Yakobo inatueleza ya kuwa hata ukipungukiwa na hekima napo unatkiwa kwenda kwa Mungu ili akupatie hekima ipitayo hekima zote za kibinadamu, ili uipokee hekima hiyo au lolote uliombalo unacho takiwa kufanya ni kuomba kwa imani timilifu..

Wagalatia 3:7; “Fahamuni basi, ya kuwa wale walio wa imani, hao ndio wana wa Ibrahimu.”

Neno linathibitisha yakuwa wale walio na imani hao ndio wana wa Ibrahimu. Kumbuka katika agano jipya tunazipata ahadi za Mungu alizo mwahidi Ibrahimu kupitia Yesu kristo kwa njia ya imani.

Unapo isoma Biblia unatambua ukweli kabisa ya kwamba Ibrahimu aliitwa baba wa imani na kuwa rafiki wa Mungu kwa sababu ya kuamini hivyo hata wewekama unahitaji kuwa rafiki wa karibu wa Mungu ni lazima utembee kwa kumwamini yeye kwa kila ulitendalo.

Kumbuka sio kuamini kwa wasiwasi bali kuamini kwa Imani timiifu isiyo na mashaka ndani yake.

Katika maombi ipo siri ya ajabu sana ambayo imefichika katika Imani kwa kile unacho taka Mungu akujibu jitahidi sana kuomba kwa imani maana pasipo imani kamwe haiwezekani kumpendeza Mungu siri hii itakusaidia sana kama utaiweka katika uhalisia wa vitendo.

Katika maisha ya wokovu nimeona majibu ya maombi yangu yakijibiwa kwa haraka sana pale nilipokuwa nikiomba kwa imani, hivyo mpendwa kama unataka kujibiwa maombi yako usihangaike kutafufuta jawabu lingine tofuti na kuomba kwa imani; maana katika imani ndimo kuna majibu tosha ya maombi yako.

Kitu kingine ninacho kushirikilisha ni kuhusu

Kuishi kikamilifu katika maisha ya wokovu maana kuna nguvu ya kipekee sana inayo chochea maombi ya imani nayo inatoka katika Roho Mtakatifu ambaye huwa ndani ya wale wote wanaoishi maisha ya kumtegemea Mungu pasipo kufuata tamaa za mwili.

Hivyo unapo ishi maisha matakatifu Roho Mtakatifu atakusukuma kuomba kwa mzingo na kwa imani katika maombi yako yote haswa yaliyo mapenzi ya Mungu kwako.

FUNGUO TATU ZA YESU ALIZOTUPA KUHUSU MAOMBI YENYE MAJIBU:

Pia kuna funguo tatu au mambo matatu ambayo Yesu ameyatoa ili kupata majibu yetu katika maombi nitaelezea moja baada ya nyingine.

1. USTAHIMILIVU (USUGU):

Funguo ya kwanza ya kujibiwa maombi ni ustahimilivu (kung’ang’ania).

Mungu anatutaka sisi kushikilia ipasavyo ahadi zake katika maombi. Maombi yetu yote yajengwe kwenye ahadi zake yeye.

Luka 11:10; “Kwa kuwa kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa.”

Sasa maana yake nini?

Omba na uendelee kuomba utapewa. Tafuta na uendelee kutafuta utapata. Bisha na uendelee kubisha mlango na utafunguliwa.

Tukimuomba Mungu ameahidi kutupa Lakini inabidi tusubirie wakati sahihi wa Mungu. Maandiko yanasema yeye hawahi wala hachelewi…

2. MAKUSUDI (BE PURPOSEFUL):

Biblia inasema sababu kubwa ya sisi kutokupokea vipawa vya Mungu ni kwa sababu hatujaomba.

Yakobo 4:2; “Mwatamani, wala hamna kitu, mwaua na kuona wivu, wala hamwezi kupata. Mwafanya vita na kupigana, wala hamna kitu kwa kuwa hamwombi!”

Zaburi 37:4-5; “Nawe utajifurahisha kwa BWANA, Naye atakupa haja za moyo wako. Umkabidhi BWANA njia yako, Pia umtumaini, naye atafanya.”

3. MAHUSIANO NA BABA (PERSONAL RELATIONSHIP):

Kitu cha muhimu sana kwenye maombi yenye majibu ni mahusiano mazuri na baba wa mbinguni.

Watu wawili kwenye biblia ambao wanasifiwa au wanaonekana kuwa na Imani kubwa ni Musa na Ibrahimu.

Lakini wawili hawa walifanikisha njia yako kwa sababu walikuwa na mahusiano ya kipekee na Mungu.

Yakobo 2:23; “Maandiko yale yakatimizwa yaliyonena, Ibrahimu alimwamini Mungu, ikahesabiwa kwake kuwa ni haki; naye aliitwa rafiki wa Mungu.”

Kutoka 33:11; “Naye BWANA akasema na Musa uso kwa uso, kama vile mtu asemavyo na rafiki yake. Kisha akageuka akarejea hata maragoni; bali mtumishi wake Yoshua, mwana wa Nuni, naye ni kijana, hakutoka mle hemani.”

Watu hawa walifanya maajabu ulimwenguni.

KWANINI WALIFANYA MAAJABU?

Lakini kumbuka inachukua muda kuwa na mahusiano ya karibu sana na Mungu.

Unaanza kwa kumhusisha Mungu kwenye mambo ya maisha yako ya kila siku.

Tenga muda maalumu kwa ajiri ya usomaji wa biblia.

Anza kuombea rafiki zako pia kumbuka kumshukuru Mungu kwa yale ambayo anajibu kila siku.

Naomba nifikie kikomo hapa kwa leo, Mungu akitujaalia wakati mwingine tutasemezana.

Bwana Mungu awabariki sana!

(Somo hili amelifundisha mtumishi wa Mungu katika platform ya group lla WhatsApp la BIBLIA NI JIBU LAKO kwenye program maalum kabisa ya mafundisho ya Neno la Mungu,tarehe 25/07/2019)