This is your very first post. Click the Edit link to modify or delete it, or start a new post. If you like, use this post to tell readers why you started this blog and what you plan to do with it.

post

Gambo Jr. Hosea

Ni Vice President na Program Coordinator (PCo.) wa huduma ya VIJANA NA UTUMISHI (tz) “Mahali kijana anajengwa kiutumishi”

UTANGULIZI:

Nawasalimia katika Jina la Yesu Kristo.

Nguvu ni nini?

NGUVU ni uwezo unaotokana na MAMLAKA. Unaweza kuwa na nguvu ya kiuchumi, inayotokana na mamlaka ya milki yako ya uchumi, ukawa na nguvu ya utawala inayotokana na mamlaka ya utawala, nguvu ya kiroho inatokana na mamlaka kiroho.

MAMLAKA ni FUNGUO zinazokuwezesha KUFUNGA au/na KUFUNGUA milango iliyo katika himaya yako. Kuna FUNGUO za aina TANO zinazotajwa na BIBLIA:-

  1. Funguo za Ufalme wa Mbinguni (MATT. 16:19)
  2. Funguo za mauti
  3. Funguo za kuzimu (UFU. 1:18)
  4. Ufunguo wa nyumba ya Daudi (ISA. 22:22, UFU. 3:7)
  5. Ufunguo wa kawaida wa mlango (AMU. 3:25)

UFUNGUO WA KAWAIDA.

Waamuzi 3: 25 – Wakangoja hata wakatahayari; na tazama, hakuifungua milango ya chumba; basi wakatwaa ufunguo, na kuifungua; na tazama, bwana wao alikuwa ameanguka nchi, naye amekufa.

Hizi funguo za kawaida ambazo kila mmoja aweza akawa anazifahamu ndiyo aina inayomaanishwa katika kitabu cha waamuzi. Funguo hizo humilikiwa na mwenye malango husika.

UFUNGUO WA NYUMBA YA DAUDI.

Isaya 22: 22 – Na ufunguo wa nyumba ya Daudi nitauweka begani mwake; yeye atafungua wala hapana atakayefunga; naye atafunga wala hapana atakayefungua.

Ufunuo wa Yohana 3: 7 – Na kwa malaika wa kanisa lililoko Filadelfia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye mtakatifu, aliye wa kweli, aliye na ufunguo wa Daudi, yeye mwenye kufungua wala hapana afungaye, naye afunga wala hapana afunguaye.

Ufunguo wa Daudi ni mmoja nao ni ufunguo wa kifalme. Nyumba ya Daudi ilipewa mamlaka (ufunguo) ya utawala (ufalme) katika Israel na Uyahudi yote. Ufunguo huu wa kifalme anaumiliki sasa Yesu Kristo, Simba na mfalme wa uzao wa Daudi kutoka kabila la Yuda.

FUNGUO ZA MAUTI NA FUNGUO ZA KUZIMU.

Ufunuo wa Yohana 1: 18 – na aliye hai; nami nalikuwa nimekufa, na tazama, ni hai hata milele na milele. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu.

Kunazo hizi funguo zaidi ya moja, funguo za mauti zipo zaidi ya moja kwa mujibu wa Biblia. Lakini pia funguo za kuzimu, nazo zipo zaidi ya moja. Yesu anasema anazo hizo funguo.

Bwana Yesu alipokufa msalabani, mwili wake ulizikwa lakini roho yake alihuishwa hata akaenda kufanya mapinduzi makubwa huko kuzimu. Huko alinyang’anya funguo za mauti na za kuzimu kutoka kwa mmiliki wa awali, shetani. Alipozichukua akawahubiri na akawafunguliwa waliofungwa.

FUNGUO ZA UFALME WA MBINGUNI.

Mathayo 16: 19 – Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lo lote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lo lote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni.

Somo letu linajikita zaidi katika hizi funguo za Ufalme wa Mbinguni. Biblia inasema, “nami nitakupa wewe…” maana yake ni kwamba Yesu Kristo ambaye ndiye mmiliki, sasa anaamua kumpa kila anayekiri ya kwamba Yesu ndiye Kristo hizo funguo za ufalme wa Mbinguni.

Kama sisi TULIOOKOKA yani tunaoamini ya kwamba YESU NDIYE KRISTO tumekabidhiwa hizi funguo, sasa tunakuwa tumekabidhiwa mamlaka ya kufungua na kufunga.

Ikumbukwe kwamba Ufalme wa Mbinguni ndiyo ufalme mkuu juu ya ufalme zote chini ya nchi, duniani na mbinguni. Ndiyo ufalme mkuu juu ya ufalme wa kila kitu, uko juu ya Ufalme wa shetani, ufalme wa mimea, wanyama, ndege, wadudu na kadhalika.

Sasa sisi TULIOKOKA tumepewa mamlaka ya kufunga na kufungua katika Ufalme huu mkuu. Maana yake ni kwamba tunaweza sasa kufunga na kufungua hata hizi falme zote chini ya ufalme wa mbinguni.

Kumbe sasa kwa huo ufunguo, ukifunga hapa duniani na mbinguni wanafunga. Hata kama shetani akienda huko kwa Mungu kukata rufaa akitaka ulicjofunga kifunguliwe, anaambiwa arudi kwako. Maana yake ni kwamba akitaka ufungue ni mpaka wewe uamue na si vinginevyo tena.

Ukikabidhiwa ufunguo wa chumba na rafiki yako, yeyote akitaka kufungua ni mpaka amfungulie na usipotaka ndiyo bass. Haleluyaaa!

Biblia inasema “Nami (Yesu) nitakupa wewe (uliyeookoka) funguo za ufalme wa mbinguni…” Maana yake siyo ufunguo mmoja bali ni zaidi ya moja.

Ukisoma Biblia utakuta kwamba zipo funguo NNE za Ufalme wa Mbinguni; ambazo ni:-

  • Jina la Yesu Kristo
  • Damu ya Yesu Kristo
  • Neno la Yesu Kristo
  • Nguvu ya Roho mtaka

Mungu akubariki sana kutembelea wavuti yetu, nakualika tena katika sehemu ya pili ya makala hii yenye nguvu ya upako wa Mungu.