ROHO MTAKATIFU DAY TWO:

Anawasilisha Mwl. Mejah Willium

BIBLIA NI JIBU LAKO

⭐biblia ni jibu lako⭐ 20180126_095329619662689..jpg

Somo hili lina sehemu mbili. Nitafundisha sehemu 1.

ROHO MTAKATIFU SEHEMU 1.

Utangulizi:

  1. ROHO MTAKATIFU NI NANI.
  2. KAZI ZA ROHO MTAKATIFU.
  3. Tabia za Roho Mtakatifu
  4. Uongozi wa Roho Mtakatifu.

ROHO MTAKATIFU NI NANI?

1. Roho Mtakatifu ni Muumbaji.

Ayubu 33:4 “Roho ya Mungu imeniumba,Na pumzi za Mwenyezi hunipa uhai.” Hii inaonesha kuwa Roho Mtakatifu ni Muumbaji.

2. Roho Mtakatifu ni Nafsi kamili

  • Anawezesha kazi ya msalaba

Waebrania 9:14 “basi si zaidi damu yake Kristo, ambaye kwamba kwa Roho wa milele alijitoa nafsi yake kwa Mungu kuwa sadaka isiyo na mawaa, itawasafisha dhamiri zenu na matendo mafu, mpate kumwabudu Mungu aliye hai?”

  • Utakaso ufanywa na Roho

1 Petro 1:2-3 “kama vile Mungu Baba alivyotangulia kuwajua katika kutakaswa na Roho, hata mkapata kutii na kununyiziwa damu ya Yesu Kristo. Neema na amani na ziongezwe kwenu.Tumaini Hai…”

  • Anawaza, anatafakari na kuomba

Warumi 8:27 “Na yeye aichunguzaye mioyo aijua nia ya Roho ilivyo, kwa kuwa huwaombea watakatifu kama apendavyo Mungu.” Acha utani na Roho Mtakatifu Roho Mtakatifu ndiyo Habari  ya mjini

  • Anao Upendo na ufurahia ushirika na mwamini.

Warumi 15:30 “Ndugu zangu, nawasihi kwa Bwana wetu Yesu Kristo, na kwa upendo wa Roho, jitahidini pamoja nami katika maombi yenu kwa ajili yangu mbele za Mungu;”

  • Anao utashi na ufanya maamuzi kama atakavyo.

3. Roho Mtakatifu ni wakala wa wokovu.

Usijisifu kwamba, “nimeokoka kwa ujanja wangu au bidii ya aliyeniongoza sala ya toba”. Sifa na utukufu ni kwa Bwana/Roho mtakatifu kwasababu moja ya kazi zake katika hili ni kuhakikisha watu wanaokoka na kufanya hayo kwa njia kuu tatu.

Ya kwanza; Kuhakikishiaulimwengu Habari ya haki, Hukumu na dhambi.

Yohana 16:7-8 “Lakini mimi nawaambia iliyo kweli; yawafaa ninyi mimi niondoke, kwa maana mimi nisipoondoka, huyo Msaidizi hatakuja kwenu; bali mimi nikienda zangu, nitampeleka kwenu. Naye akiisha kuja, huyo atauhakikisha ulimwengu kwa habari ya dhambi, na haki, na hukumu.”

Ya Pili; Kufundisha ulimwengu Habari za wokovu Yaani kuhusu Kristo.

Yohana 14:26 “Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia.”

Sasa kuanzia leo usiseme Mimi naokoa watu, sema Roho Mtakatifu ndani yangu ndiye anaokoa watu. Yeye ni Roho Wa Neema. Walokole wenzangu bhana… mtu anafanya jambo baada ya kumpa Mungu Roho Ndani yake. Utasikia, “nikasikia kitu kinaniambia moyoni.” Usiseme kitu Sema Roho Mtakatifu.

Watumishi nafundisha mseme ukweli kabisa Roho Mtakatifu ni engine ya kila Mkristo.

Ya Tatu; Roho Mtakatifu utupa kuzaliwa mara ya pili.

4. Roho Mtakatifu ni wakala wa utakaso.

Hakuna Utakatifu bila Roho Mtakatifu. Juzi nilikuwa Moro nilikutana na watu wa kanisa flani wao hawaamini katika Roho Mtakatifu na pombe wanapiga kama kawaida

Waroma 8:1 “Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu. Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti. Maana yale yasiyowezekana kwa sheria, kwa vile ilivyokuwa dhaifu kwa sababu ya mwili, Mungu, kwa kumtuma Mwanawe mwenyewe katika mfano wa mwili ulio wa dhambi, na kwa sababu ya dhambi, aliihukumu dhambi katika mwili;”

  • Anatuita na kutukumbusha kwamba sisi ni watoto wa Mungu.

“Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu;” Warumi 8:16 SUV

  • Hutusaidia katika Ibada yetu na Mungu.

Matendo 10:46 “Kwa maana waliwasikia wakisema kwa lugha, na kumwadhimisha Mungu. Ndipo Petro akajibu,”

Tujifunze kidogo Roho Mtakatifu yukoje nasi?

  • Yupo pamoja nasi.

Joel 2:28 “Hata itakuwa, baada ya hayo, ya kwamba nitamimina roho yangu juu ya wote wenye mwili; na wana wenu, waume kwa wake, watatabiri, wazee wenu wataota ndoto, na vijana wenu wataona maono;”

Angalizo: Roho Mtakatifu hakai katika Mioyo michafu, mioyo ya watenda dhambi, mioyo miovu.

  • Yupo Ndani yetu.

Na hapa anafanya kazi ya kutuletea wokovu.

Warumi 8:9 “Lakini ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake.” Pia soma na Yohana 3:3-6

“Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu. Nikodemo akamwambia, Awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee? Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa? Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu. Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho.” Yohana 3:3-6 SUV

  • Huwa anakuja juu ya Mtu.

Na hapa ni kwa ajili ya kutimiza kusudi flani. Pia hapa anaweza kuwa ni kwa ajili ya kufanya kazi/project flani ya Mungu.

Mfano mzuri ni Jinsi Roho Mtakatifu alivyokuwa juu ya Mariamu kwa ajili ya kumbeba Yesu mkombozi wa Ulimwengu.

Waweza soma zaidi Mdo 1:8, Luka 24:49 na Mdo 10:38

Sisi tunaamini katika Roho Mtakatifu lakini lazima ujue hata ulimwengu wa giza unaye roho wao anayeitwa roho wa utambuzi.

KAZI ZA ROHO MTAKATIFU

Hapa sitaelezea sana na nitajitahidi nisirudie za jana maana nimefuatilia somo la Jana Mtumishi kaelezea Kweli kweli

Ngoja niongezee chache tu.

  1. Kuvunja pingu na vifungo

2wakorintho 3:17 Basi “Bwana” ndiye Roho; walakini alipo Roho wa Bwana, hapo ndipo penye uhuru.

Luka 4:18-19 “Roho wa Bwana yu juu yangu,Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao,Na vipofu kupata kuona tena,Kuwaacha huru waliosetwa, Na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa.”

Isaya 10:I2 “Tena itakuwa katika siku hiyo mzigo wake utaondoka begani mwako, na nira yake shingoni mwako, nayo nira itaharibiwa, kwa sababu ya kutiwa mafuta.”

  1. Kuusulubisha mwili na tamaa zake.

Ukiona mkaka kila akiona binti anageuza shingo ujue hapo Roho Mtakatifu yupo likizo.

Warumi 8:5-9 “Kwa maana wale waufuatao mwili huyafikiri mambo ya mwili; bali wale waifuatao roho huyafikiri mambo ya roho. Kwa kuwa nia ya mwili ni mauti; bali nia ya roho ni uzima na amani. Kwa kuwa ile nia ya mwili ni uadui juu ya Mungu, kwa maana haitii sheria ya Mungu, wala haiwezi kuitii. Wale waufuatao mwili hawawezi kumpendeza Mungu. Lakini ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo”

Huwezi kuwa na Roho Mtakatifu ukaanza kijana unasikiliza nyimbo za Dunia, ukaanza kutazama picha za utupu, kwenye watsapp umejiunga makundi ya ex, unavaa vimini hadi kanisani, unasalimiana na mtu wa jinsia tofauti unamkumbatia dakika 10.

Kama ilivyo Jina lake Roho Mtakatifu Asili yake ni Mtakatifu.

Warumi 7:15-18 “Maana sijui nifanyalo, kwa sababu lile nilipendalo, silitendi; bali lile nilichukialo ndilo ninalolitenda. Lakini kama nikilitenda lile nisilolipenda, naikiri ile sheria ya kuwa ni njema. Basi sasa si mimi nafsi yangu ninayetenda hilo, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu. Kwa maana najua ya kuwa ndani yangu, yaani, ndani ya mwili wangu, halikai neno jema; kwa kuwa kutaka nataka, bali kutenda lililojema sipati”

Wakati ninazungumzia nikakumbuka ninasomo Roho Mtakatifu alinifundisha kuhusu tamaa na hisia. Nafikiri itakuwa package nzuri kwa vijana wenzangu.

Hili Swala la Tamaa linasumbua hasa nyie mlioko chuoni huko bila Roho Mtakatifu ni shida. Unaenda discusion unategwa Unakuta nawe umeanguka.

  1. Kutuwezesha kukua Kiroho

2 Wakorintho 3:6 “Naye ndiye aliyetutosheleza kuwa wahudumu wa agano jipya; si wa andiko, bali wa roho; kwa maana andiko huua, bali roho huhuisha.”

  1. Kutunyakua kwenda Mbinguni.

Kutubadili asili yetu. Soma hii, naelezea chini

Luka 1:34 “Mariamu akamwambia malaika, Litakuwaje neno hili, maana sijui mume? Malaika akajibu akamwambia, Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli; kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu. Tena, tazama, jamaa yako Elisabeti naye amechukua mimba ya mtoto mwanamume katika uzee wake; na mwezi huu ni wa sita kwake yeye aliyeitwa tasa; kwa kuwa hakuna neno lisilowezekana kwa Mungu.”

Ni hivi Roho Mtakatifu ndiye alimpa nguvu Mariamu za kumzaa mwokozi Yesu ambaye tukimfuata yeye ni njia ya kuelekea Mbinguni.

Hili andiko mimi huwa nalipenda. Ebu litafakari kama mimi leo ni hivi. Yaani Roho Mtakatifu alimwezesha mariamu kumzaa Yesu na Yesu baada ya kuachilia wokovu alituachi msaidizi ambaye ni Roho Mtakatifu.  Yaani Roho Mtakatifu usimtazame kwa namna za kawaidia bila Roho Mtakatifu hakuna wokovu, utakaso, uzima hadi uumbaji.

Nashangaa mtu ameokoka ajaona Roho Mtakatifu akumpigania na anasikia amani.  OMBA LEO KWAMBA ROHO MTAKATIFU NATAKA KUONA UKIGUSA MAISHA YANGU LEO.

HAPA najua utanielewa nacho maanisha kuwa Roho Mtakatifu ni Roho wa Unyakuo.

Matendo 8:38-40 “Akaamuru lile gari lisimame; wakatelemka wote wawili majini, Filipo na yule towashi; naye akambatiza. Kisha, walipopanda kutoka majini, Roho wa Bwana akamnyakua Filipo, yule towashi asimwone tena; basi alikwenda zake akifurahi. Lakini Filipo akaonekana katika Azoto, na alipokuwa akipita akahubiri Injili katika miji yote, hata akafika Kaisaria.”

  1. Kutusaidia kuabudu katika Roho na Kweli.

Bila Roho Mtakatifu utajikuta unaimbia uzoefu tu watu pamoja na Mungu akuna anayeguswa na huduma yako. Utaimba lakini unaishia kuitwa mwanakwaya au siku hizi tunawaita praize time lakini ukibarikiwa kidogo ni kupata Mchumba ambaye hata mapenzi hayadumu au kupewa cheo kwenye Praise team.

Ndugu lazima kuwa na Roho Mtakatifu. Soma hapo utajua ninacho maanisha

Yohana 4:23 “Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu. Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.”

Tusijifanye tunampenda au tunamtii Roho Mtakatifu maana kiwangocha utii wa Roho Mtakatifu kinategemea haya mambo matatu;

  1. Kuitambua sauti yake. Sasa kama humtambui utamtiije.
  2. kusikia sauti yake. Wewe kama ni kiziwiwa Kiroho Uwezi msikia Roho Mtakatifu.
  3. Kuitii sauti yake.

Na hizo ndizo chache kati ya Tabia zake. Pona yako Mtumishi hipo katika kutambua, kutathmini na kumsikiliza Roho Mtakatifu. Usiwe Mzembe katika kuomba Ujazo wa Roho Mtakatifu na kutafuta maarifa kuhusu Roho Mtakatifu.

UONGOZI WA ROHO MTAKATIFU

Nitakwenda haraka Kidogo katika hili lakini najua baada ya hii maswali yatapungua. Maana watu wengi wamekuwa wakidanganywa na kudanganya.

Mfano: Mtu anasema Roho Mtakatifu kanionesha ni wewe nk

Katika kuongozwa na Roho kuna namna mbalimbali. Siyo kila Anayeongozwa na Roho anapata Ndoto au anamwona Roho Mtakatifu anashuka na kuongea naye HAPANA Kuna njia nyingi sana. Baadhi ni hizi.

  • Kwa njia Maono

Anania wala hakuwa katika Ndoto alipata maono kutoka kwa Mungu.

Matendo 9:10 “Basi palikuwapo Dameski mwanafunzi jina lake Anania. Bwana akamwambia katika maono, Anania. Akasema, Mimi hapa, Bwana. Bwana akamwambia, Simama, enenda zako katika njia iitwayo Nyofu, ukaulize katika nyumba ya Yuda mtu aitwaye Sauli, wa Tarso; maana, angalia, anaomba;”

  • Neno la Maarifa

1 Wakorintho 12:4-8 “Basi pana tofauti za karama; bali Roho ni yeye yule. Tena pana tofauti za huduma, na Bwana ni yeye yule. Kisha pana tofauti za kutenda kazi, bali Mungu ni yeye yule azitendaye kazi zote katika wote. Lakini kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa kufaidiana. Maana mtu mmoja kwa Roho apewa neno la hekima; na mwingine NENO LA MAARIFA apendavyo Roho yeye yule.”

Kwa hiyo Roho Mtakatifu anaweza kupitisha Neno la maarifa akakuongoza kusoma sehemu fulani au akapitisha Neno madhabahuni. Tatizo walokole tunafikiri Roho Mtakatifu anatumia Njia moja tu,.

  • Neno la Hekima.

Soma hiyo hiyo 2Korintho 12 limeelezea.

Mfano; Mungu anaweza pitisha Neno la Hekima watu wakiwa kwenye kikao Jibu limekosa Mtu anasema Neno moja likawapa solusion.

Kwa hiyo sasa usikariri kwamba mwenye Roho Mtakatifu ni yule tu anayesema nimeona nimeona mu Roho asema. Tuwe makini sana. Nashukuru jana mwl alizungumzia Huduma, Karama na vipawa vya Roho Mtakatifu.

  • Kwa njia ya Ndoto.

Roho Mtakatifu anatumia Ndoto pia kama niliyosema hapo juu. Kwamba siyo njia pekee.

Na Ndoto watu wa Mungu siyo zote zinatoka kwa Roho Mtakatifu nyingine zinatoka kwa shetani. Nyingine zinatokana na matendo yetu yanayochukua nafasi.

Mfano: Mtu anakwambia Mimi naota nikiwa na zini lakini ukimfuatilia. Unakuta alilala saa 8 usiku anachati na wanaume/wanawake. Au analala anatazama love story movies.

Ndoto zipo na zina maana tofauti tofauti. Hasa wanachuo mabinti wanapenda sana tamthilia aisee. Mkaka saa 9 usiku. Duh

Mathayo 2:19-21 “Hata alipofariki Herode, tazama, malaika wa Bwana alimtokea Yusufu katika ndoto huko Misri, akasema, Ondoka, umchukue mtoto na mamaye, ushike njia kwenda nchi ya Israeli; kwa maana wamekufa walioitafuta roho ya mtoto. Akaondoka akamchukua mtoto na mamaye, akafika nchi ya Israeli.”

  • Kwa ushuhuda wa Moyoni. (Sauti ya Ndani)

Isaya 55:8-11.

Mfano: Ulishawahi kuona unaombea Jambo mad mrefu alafu inatokea hali fulani au Unakutana na Hali fulani ulilinganisha na ulichokuwa unakiomba Unaona kabisa ni Mungu mwenyewe.

Kuna wakati unasikia msukumo moyoni either kufanya kitu fulani au kutofanya Jambo fulani.

Sasa kama wewe unasuniri tu Roho Mtakatifu aje umuone anatembea na kukuongelesha to utasubiri sana zipo njia Nyingi.