Merito Tagalile
~0657 048393
~0625 610925

Mungu hapendi mtu yoyote apotee ndio maana akamuachilia Yesu Kristo atufie msalabani kwaajili ya dhambi zetu

Ndio maana akasema kwamaana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa mwana wake wa pekee ili kila mmoja asipotee bali awe na uzima wa milele, Yohana 3:16

Ijapokuwa tumepewa upendeleo huo lakini hatuufuati, tuwe wakweli wa Kristo tumekua wavivu katika kuitenda kazi ya Mungu na kuwatoa watu kwenye Giza na kuwaleta nuruni,

Leo nilipokua nasoma Kitabu cha waamuzi nikaona vile Mungu alivyowapenda wana wa Israel, lakini wana wa Israel wakawa wanafanya machukizo kwa kujichanganyisha katika madhabahu na uchafu wa mataifa, na kipindi Kile kuabudu miungu ya mataifa ilikua dhambi kubwa kwakua aliwaapia waisrael wasichangamane na uovu wa mataifa watakayo ishi ndani yao, Waamuzi 2:11:23

Ukitafakari Yale mambo kwamakini utaona kabisa sasa hivi wengi wao wanayafanya hayo wakichukulia kawaida, wakiona ni vitu vidogo havina athali yoyote kiroho kumbe vinaathali kubwa, Galatia 5:19-21

Ndio maana unaskini umekithili, mahangaiko yamekithili kwa watu, sio kwamba Mungu haon hapana anawaacha watu wapigwe kwakua wamekataa kufuata njia zake, badala yake wanafuata ya ulimwengu

Ametufanya kuwa wafalme na makuhan ili tumiliki na kutawala lakini hatusimami katika zamu za ukuhan na ufalme, Ufunuo 5:9-10 badala yake tunasimama kama watu tusio wathaman mbele za Mungu,na katika jamii zetu, tupo kama yatima na tumejenga akili zetu kuwa sisi niwatu dhaifu.

Upo kwenye mtaa wako ili kuondoa uovu uliosimama kwenye jamii yako, Yeremia 1:10, Yeremia 51:20-23, huwezi kuuondoa ikiwa huna Maombi mazito na endelevu, ndio maana adui anatawala na maovu yanaongezeka sababu tumeacha kusimama kwenye nafasi zetu, Mungu aliposema hakutaka mtu apotee ni ili tulio okoka tusimame kuitangaza Injili kupitia Maombi na kulitangaza Neno.

Asikwambie mtu hiyo kazi ninzuri ikiwa huufuati mwili unaposema nimechoka, songa mbele katika maombi, simama ili mtaa, jamii yako na NCHI yako ipone.

Nakutakia tafakari njema ya kulitenda kusudi la Mungu, kumbuka ukiwa dhaifu utakwenda kujibu mbele za Mungu kwakua amekupa nguvu, amekupa uwezo amekupa mamlaka lakini vyote hivi unapotezea na kufanya yakwako, mwisho wake unaishia kuhangaika na kuteseka.

Ubarikiwe na uwe mtu wa kujitafakari.

Kama umebarikiwa na ujumbe huu share kwa ndugu jamaa na rafiki zako popote pale facebook na kwenye magroup ya Whatsup hutaachwa hivyo hivyo bali utabarikiwa kwa kuitangaza injili kwa kushare.

Ukipenda kutumiwa masomo ya Neno la Mungu kila siku kwa Whatsup tuma majina yako mawili inbox, whatsup kwa namba ya Tigo 0657 048393 kuomba kuunganishwa kupewa masomo kila siku na utatumiwa, pia kwa ushauri na maombi piga namba zilizopo hapo chini, na Mungu wambinguni akubariki sana.