PRESENTED BY MWL. WILLIAM MEJAH, DA ES SALAAM.

Tarehe 27 December 2017.

SIKU YA KWANZA YA SEMINA YA MAOMBI TR 27/12/2017

mylogo20171203083016-2111862196.png

Karibu Kwenye semina watu wa Mungu. Nafungua semina hii katika Jina la YESU KRISTO WA NAZARET.

Kwa Majina naitwa William Mejah. Napatikana Dar es Salaam.

DAY ONE SEMINAR 27/12/2017

Karibu Kwa masaa Haya matatu (1500hrs-1800hrs) naamini utapata kitu. Ratiba niliyonayo ina sehemu TATU zenye dakika 45; sehemu ya kwanza (1500hrs-1545hrs), sehemu ya pili (1600hrs-1645hrs) na sehemu ya mwisho (1700hrs-1745hrs). kila baada ya sehemu moja kuna dakika 15 za mapumziko.

Somo hili la maombi lina sehemu kuu TANO kama zifuatavyo:

  1. Aina za Maombi.
  2. Style za kuomba.
  3. Mbinu za Kuomba.
  4. Mikao tofauti ya kuomba.
  5. Namna ya kupokea Maombi yako.

Tufuatane Ili uweze kujifunza. Usikubali kupitwa na point yoyote.

Kwa leo nitaanza na AINA ZA MAOMBI. Hapo kwenye style na mikao ni kama majina yanafanana lakini Kuna tofauti. Tukipata Neema ya kufika huko nafikiri utanielewa.

Kitabu cha kujifunzia ni Biblia (Bible is our reference book).

Maombi ni nini?

Maombi ni namna ya kwenda katika ulimwengu wa Roho kuadhiri ulimwengu wa Roho na kuleta katika Ulimwengu wa Mwili. Sitaelezea “ulimwengu wa Roho” kwa leo lakini ujue upo ulimwengu wa Roho na huko Ndiko Mungu wetu anapopatikana.

Kwa maana nyingine; Maombi ni mawasiliano kati ya mwombaji na Mungu wake. Kwa hiyo fahamu kwamba hatuombi kwa sababu ya matatizo bali ni mawasiliano na Mungu wetu.

Yesu hakuwa na matatizo lakini aliomba. Luka 6: 12 “Ikawa siku zile aliondoka akaenda mlimani ili kuomba, akakesha usiku kucha katika kumwomba Mungu.”

Yesu aliamka asubuhi na Kwenda kuomba. Marko 1: 35 “Hata alfajiri na mapema sana akaondoka, akatoka akaenda zake mahali pasipokuwa na watu, akaomba huko.” Paulo anatuambia katika Waefeso 6: 18 “kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote;”

Ulikuwa ni utangulizi hebu twende sasa kwenye Aina za Maombi.

Aina za Maombi.

Aina hizi ni kwa Jinsi nilivyofunuliwa Mtu mwingine anaweza kuwa na Aina nyingi zaidi. Tutaziangalia aina hizi zifuatazo SITA:-

  1. Maombi ya maombezi
  2. Maombi binafsi.
  3. Maombi ya vita.
  4. Maombi ya Sifa.
  5. Maombi ya Shukrani.
  6. Maombi ya Toba.

A) MAOMBI YA MAOMBEZI:

Maombi ya Maombezi ni Maombi kwa ajili ya watu wengine. Maombi kwa ajili ya kuombea watu wengine, kuombea Huduma, kuombea kanisa. Mchungaji au Mtumishi kuombea wenye mahitaji hayo ndiyo kuitwa Maombi ya maombezi.

Kwa hiyo ni wajibu wetu kuombea watu wengine. Kuombea Nchi, Viongozi wetu.

Ukisha kuwa umeokoka unapewa kumiliki, kutawala na kutiisha. 1Timotheo 2: 1-3 “Basi, kabla ya mambo yote, nataka dua, na sala, na maombezi, na shukrani, zifanyike kwa ajili ya watu wote; kwa ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka, tuishi maisha ya utulivu na amani, katika utauwa wote na ustahivu. Hili ni zuri, nalo lakubalika mbele za Mungu Mwokozi wetu;”

Wakristo wengi hatuombei wengine, tunapenda kujiombea.  Hivi ulishawahi kufunga kwa ajili ya Mtu mwingine au Nchi yako?

Ulishawahi kwenda kwenye Maombi ukaombea watu wengine bila kujitaja? Tunatakiwa kubadilika na kuwapenda wengine kama Nafsi zetu. Kutoombea wengine ni Ubinafsi na Ubinafsi ni DHAMBI

Kwa nini tuombee watu wengine?

  • Yesu alituombea lazima nasisi tuombee wengine.
  • Ili kuwe na Amani. Ukiombea Viongozi wataongoza Nchi kwa Amani. Amani ya Nchi inategemea Maombi yako. Maombezi yanaleta Amani; Isaya 59:16 “Akaona ya kuwa hapana mtu, akastaajabu kwa kuwa hapana mwombezi; basi, mkono wake mwenyewe ndio uliomletea wokovu; na haki yake ndiyo iliyomsaidia.” Lazima kupanda Maombi kwa ajili ya watu wengine.
  • Nguvu za Israeli ni kwa sababu ya kabila la lawi lililokuwa limetengwa kuwa waombezi. Kumbukumbu la Torati 10;8-9 “Na wakati huo BWANA aliitenga kabila ya Lawi ili walichukue lile sanduku la agano la BWANA, wasimame mbele ya BWANA kwa kumtumikia, na kuwabarikia watu kwa jina lake, hata hivi leo. Ndipo asiwe na fungu Lawi, wala urithi pamoja na nduguze; BWANA ndiye urithi wake, kwa mfano wa vile alivyomwambia BWANA, Mungu wako.)”
  • Mungu anatafuta mwombezi wa kuombea Nchi. Ezekieli 22: 30 “Nami nikatafuta mtu miongoni mwao, atakayelitengeneza boma, na kusimama mbele zangu mahali palipobomoka, kwa ajili ya nchi, nisije nikaiharibu, lakini sikuona mtu.”

Tumalizie Aina hii ya Maombi ya Maombezi.tunaona ni lazima Ujue kwamba Mimi na wewe ndiyo Walawi kwa ajili ya Nchi yetu na hata Jamii yetu.

Lawi lilikuwa ni kabila ambalo lilikuwa limetengwa kwa ajili ya kuombea Israel. 2Nyakati 7: 14 “ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao.”

Vitu vya kuzingatia Unapofanya Aina hii ya Maombi;

  • Omba Uongozi wa Roho Mtakatifu.
  • Mzigo/Utungu/kiu kutoka Kwa Bwana.
  • Neno la Mungu.
  • Moyo wa huruma.

Maombi yako lazima yatokane na Neno la Mungu. Mungu ni Neno. Bila kuona mzigo kwa ajili ya Nchi au mwitaji ni Ngumu kumwombea. Yohana 1:1 “Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.”

Lazima kuwa na Moyo wa huruma kuweza kuombea wengine.

  • 2Korintho 3:4
  • Mwanzo 19:13-29
  • Marko 5:1-20
  • Waefeso 4:17-20.

Mwisho katika hii Aina ya Maombi ni Juu ya kuombea watumishi. Tumezoea kuombewa na watumishi lakini Kuna sababu za sisi kuombea watumishi.

Upako, ufanisi na Nguvu za Mtumishi zinategemea na wewe hasa katika Aina hii ya Maombi. Tunatakiwa kuwaombea watumishi kwa sababu leo anaweza kuwa mzuri na Kesho akaonenana mbaya.

Kuna wakati Mtumishi anaweza kuingiliwa na Roho mbaya

Luka 9:54-56 “Wanafunzi wake Yakobo na Yohana walipoona hayo, walisema, Bwana, wataka tuagize moto ushuke kutoka mbinguni, uwaangamize; [kama Eliya naye alivyofanya]? Akawageukia, akawakanya. [Akasema, Hamjui ni roho ya namna gani mliyo nayo.] Kwa maana Mwana wa Adamu hakuja kuziangamiza roho za watu, bali kuziokoa. Wakaondoka wakaenda mpaka kijiji kingine.Wafaao kuwa Wafuasi wa Yesu”

Mfano 2; Petro alikuwa Mwema sana lakini ghafla alibadilika na kuwa mbaya. Ukijua hivi vitu hutaacha kuombea watumishi. Hapa Petro alikuwa Mwema sana.

Mathayo 16: 17 “Yesu akajibu, akamwambia, Heri wewe Simoni Bar-yona; kwa kuwa mwili na damu havikukufunulia hili, bali Baba yangu aliye mbinguni. Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.”

HAPA Petro akaonekana Mbaya. Akaitwa shetani. Mathayo 16: 22 “Petro akamchukua, akaanza kumkemea, akisema, Hasha, Bwana, hayo hayatakupata. Akageuka, akamwambia Petro, Nenda nyuma yangu, Shetani; u kikwazo kwangu; maana huyawazi yaliyo ya Mungu, bali ya wanadamu.Msalaba na Kujikana. Wakati huo Yesu aliwaambia wanafunzi wake, Mtu ye yote”

Kwa hiyo tunapaswa kutumia Aina hii ya Maombi. Ndiyo mwisho wa Aina hii nafikiri umepata kitu.

B) MAOMBI BINAFSI (Private prayer):

Ni kukumbushe kwamba Maombi ni namna ya kuingia katika ulimwengu wa Roho kuathiri na kuleta katika ulimwengu wa Mwili. Kwa hiyo Maombi ni njia moja wapo ya kuingia Rohoni.

Ngoja nikutajie pamoja na njia zingine za kuingia katika ulimwengu war oho, japo ni nje ya mada lakini ni vizuri uzifahamu na kuzifuatilia.

Maombi binafsi kwa lugha nyingine yanaitwa maombi ya mahitaji. Neno Maombi linatokana na Neno Omba. Kuomba maana yake unakuwa na uhitaji. Lazima uone kuwa unauhitaji ndipo UOMBE aina hii ya Maombi. Unapokwenda mbele za Mungu inatakiwa kuwa specific (Muwazi) Mungu hawezi potezea hisia zako hata siku moja na hajawahi.

MITHALI 28: 13 “Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema.”

Kwa hiyo unapoingia kwenye Maombi Binafsi mweleze Mungu ukweli acha kuvunga. Mungu anajua haja zako hata Kabla ya kuomba. Warumi 8:32 “Yeye asiyemwachilia Mwana wake mwenyewe, bali alimtoa kwa ajili yetu sisi sote, atakosaje kutukirimia na mambo yote pamoja naye?”

Tuangalie Kidogo biblia inatuambia nini kuhusu Maombi Binafsi. Soma hii Mistari hapa chini.

Zaburi 145:18-19 BWANA yu karibu na wote wamwitao,Wote wamwitao kwa uaminifu. Atawafanyia wamchao matakwa yao,Naye atakisikia kilio chao na kuwaokoa.

Zaburi 37:4 Nawe utajifurahisha kwa BWANA,Naye atakupa haja za moyo wako.

Wafilipi 4:6-7 Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu. Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu.

Mathayo 6:11 Utupe leo riziki yetu.

Baba hakupi pilau hata kama pilau hipo. Anakupa sawa na ulivyoomba. Jizoeze kuomba vitu vikubwa vikubwa acha kujidharau.

Yohana 16:24 Hata sasa hamkuomba neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata; furaha yenu iwe timilifu.

Jizoeze kuishi maisha ya Maombi.  Omba kwa Jina la Yesu. Unapofanya aina hii ya Maombi weka Imani yako katika Jina la Yesu. Marko 10:28-30 “Petro akaanza kumwambia, Tazama, sisi tumeacha vyote tukakufuata wewe. Yesu akasema, Amin, nawaambieni, Hakuna mtu aliyeacha nyumba, au ndugu waume, au ndugu wake, au mama, au baba, au watoto, au mashamba, kwa ajili yangu, na kwa ajili ya Injili, ila atapewa mara mia sasa wakati huu, nyumba, na ndugu waume, na ndugu wake, na mama, na watoto, na mashamba, pamoja na udhia; na katika ulimwengu ujao uzima wa milele.”

Vitu Unavyotakiwa kuzingatia katika Aina hii ya Maombi:

➖Jina la Yesu.

➖Neno la Mungu.

Katika kila Maombi lazima kutumia Neno. Maombi siyo wingi wa maneno bali Neno. Kilicho msaidia Ibrahim ni kwamba aliweka Imani yake katika Neno. Hakuwa na mzaha na Neno la Mungu.

Mwisho wakati unafanya aina hii ya Maombi lazima kuhakikisha Imani yako haijengeki au kushikilia sana haya mambo yafuatayo Japo ni Muhimu.

  • Imani yako isikae katika saa au wakati wa Kuomba. Usikalili mda wa Kuomba kuwa tayari mda wowote. Kuwa tayari saa yoyote. Usisubili mda wa kulala,kuamka au jumapili kanisani. Omba bila kukoma.
  • Imani isikae katika urefu wa Muda wa Maombi. Ni vizuri kuomba Mda mrefu na Mimi nasisitiza Maombi ya mda mrefu. Kuomba mda Mrefu kunakuwa na Maana pale unapoomba sawa sawa na Neno la Mungu. Maombi yasiyotokana na Neno ni makelele mbele za Mungu.
  • Imani yako isikae katika mahali pa kuomba. Ukikariri sehemu utakwama siku ukisafiri. Ukiwa eneo lolote Omba ikibidi kukemea kemea.
  • Imani yako isikae katika Mtu anayekuombea. Watu wengine Mpaka Mtu fulani amwombee. Yaani asipokuwapo huyo yeye haombi. Jizoeze Maombi Binafsi. Amelaaniwa amtegemeaye Mwanadamu.
  • Imani yako Usiwe katika sauti fulani. Hata ukilia kama hauombi sawa na mapenzi ya Mungu ni kazi bure. Usiamini katika sauti ya juu, ya chini au kulia. Omba sawa sawa na mapenzi ya Mungu.
  • Imani yako isiwe katika kufumba macho. Kuna wakati utatakiwa kukemea pepo Kuna wakati utakua unaendesha UOMBE n.k
  • Imani yako isiwe katika ukubwa wa tatizo. Hapa ngoja nielezee Kidogo. Usiombe kulingana na ukubwa wa tatizo. Kuna watu wakiwa na matatizo wanaomba lakini bila tatizo wala haombi. Mtu akiwa na mtihani au akiwa anatafuta mchumba anakesha hadi kanisani lakini akipata anatulia.

Siku nyingine Funga na kuomba kwa ajili ya kushukuru tu.  Tena siku hiyo upeleki hoja yoyote bali kushukuru.

Mda uliobaki hautoshi na hauniruhusu kumalizia lakini itoshe kusema Haya ndiyo Mungu aliyokuaudia siku hii ya leo.

MASWALI

  1. Ninapenda kuuliza kutokana na maombi ya kibinafsi. Je nivibaya kushirikiana na mtu mwenzio kwa kuombea hitaji lako binafsi?

Majibu;

Kama umefuatilia Maombi ya Maombezi nimesisitiza juu ya kuombeana. Kuombea wengine

Amina siyo vibaya kumshirikisha mtu mwingi maana Bwana asema walipo wawili watatu kwa jina langu mi nipo pamoja nao.

  1. Ukiomba bila kuambatanisha neno maombi yako hayatapokelewa na Mungu?

Majibu;

Ndiyo; Maombi lazima yatokane na Neno la Mungu. Mungu mwenyewe ni Neno. Hii inasaidia kuondoa Tabia za kukariri sala Ile Ile kila siku.

  1. Kuna wakati mtu anaomba sana siku nyingi ila hapati jibu je inatokana na musimamo anao mbele za Mungu ao inatokana na dhambi anaweza kuwa alitenda miaka ya mbele?

Majibu;

Ndiyo hizo zote zinaweza kuwa ni sababu. Sikuweza kufikia kipengele cha kutojibiwa kwa Maombi.

Lakini kwa Ufupi kutojibiwa kwa Maombi yetu Baadhi ya sababu.

  1. Dhambi -Mioyo inayokataa Toba.
  2. Imani – Pasipo Imani hatuwezi kumpendeza Mungu – Waebr 11:6.
  3. Nguvu haba – Mungu anatumia Nguvu zilizopo ndani yetu kujibu maombi (Waef 3:20)
  4. Kukosa uvumilivu – Wengine wanataka akiomba leo ajibiwe leo.
  5. Kuomba kitu ambacho siyo halali yako. AU
  • Utakatifu (Mungu anapenda Moyo wa Utakatifu Yaani toba). Isaya 59:1-2; Isaya 1:15-19; Kumb 23:14.
  • (Mungu anachukia Mioyo yenye kuona shaka) 1yonaha 3:18-19.
  • (Nia yako lazima iwe njema). Yakobo 4:2-3.
  • warumi 8:7
  • Ukiona kanisa halifundishi kutoa sadaka hama haraka sana. Sadaka ni Muhimu sana. Yakobo 5:16-18